BAGHDAG. Mauaji yazidi Iraq.
22 Aprili 2005Kikundi kinachojiita Jeshi la Kiislamu nchini Iraq kimetangaza kuhusika na udenguaji wa ndege aina ya helicopta mali ya nchi ya Bulgaria hapo jana ambapo watu 11 waliuwawa wakati ndege hiyo ilipokuwa ikiruka kutoka mji mkuu wa Baghdad ikielekea Tikrit ilipolengwa na kombora la Gruneti.
Kundi hilo la waislamu wenye siasa kali lilionyesha ukanda wa video ulioonyesha mabaki ya ndege hiyo na miili ya watu iliyo tapakaa na likadai pia kumteka nyara mmoja wa watu hao na kumuua.
Kampuni iliyomiliki ndege hiyo imetoa taarifa kuwa watu waliokufa ni wahudumu wa ndege hiyo wabulgaria 3 abiria 6 wamarekani na walinzi wawili wa kifilipino.
Katika tukio jingine polisi mjini Baghdad wametoa taarifa ya kuuwawa watu wanane na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulizi la bomu lilotegwa ndani ya gari mchana wa leo wakati sala ya ijumaa ilipokuwa ikiendelea katika msikiti wa madhehebu ya Shia wa Al Subeih mashariki mwa mji wa Baghdad.