BAGHDAD:Waziri wa Ulinzi Iraq aanzisha Operesheni kabambe ya usalama Baghdad
26 Mei 2005Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Iraq Sadoun al- Dulaini ametangaza opareresheni kabambe ya usalama itakayofanywa na zaidi ya wanajeshi elfu 40 wa Iraq katika mji wa Baghdad.
Akizungumza katika mkutano Sadoun alisema vikosi hivyo vitavijumuisha pamoja vikosi kutoka wizara za mambo ya ndani na Ulinzi.
Oparesheni hiyo dhidi ya waasi ndio kubwa zaidi kuwahi kufanywa na vikosi vya usalama vya Iraq.
Wakati huo huo waziri wa mambo ya ndani wa Iraq amethibitisha habari kwamba Gaidi kutoka Jardan Abu Musab Al Zarqawi amejeruhiwa vibaya katika operesheni ya wanajeshi wa Marekani.