BAGHDAD:Waziri mkuu wa Iraq Jaafar awasilisha orodha ya watakao kuwa mawaziri wapya bungeni
27 Aprili 2005Matangazo
Waziri mkuu mteule nchini Iraq,Ibrahim Al Jaafar ametoa orodha ya watakaokuwa mawaziri katika serikali yake. Hatua ya bwana Jaafar imekuja baada ya wiki kadha za mazungumzo yaliyolenga kuunda serikali ya mseto nchini humo, lakini haijabainika ni lini ataunda serikali.
Wakati huo huo makundi ya kisiasa ya wasunni waliowachache yanadai kupewa mdaraka katika wizara muhimu ili kuwepo usawa katika ugavi wa mamlaka kati ya washia na wakurdi. Habari nyingine zinasema kuwa mbunge mmoja ameuwawa mjini Baghdad.
Polisi nchini humo wanasema mwanachama wa serikali ya muda ya Iyad Allawi ameuwawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake.