BAGHDAD.:Waziri mkuu wa Iraq atoa orodha ya mawaziri wapya
27 Aprili 2005Matangazo
Waziri mkuu mteule nchini Iraq,Ibrahim Al Jaafar ametoa orodha ya watakaokuwa mawaziri katika serikali yake. Hatua ya bwana Jaafar imekuja baada ya wiki kadha za mazungumzo yaliyolenga kuunda serikali ya mseto nchini humo, lakini haijabainika ni lini ataunda serikali.
Wakati huo huo makundi ya kisiasa ya wasunni waliowachache yanadai kupewa mdaraka katika wizara muhimu ili kuwepo usawa katika ugavi wa mamlaka kati ya washia na wakurdi. Wasunni walikuwa na uhuru mkubwa wakati wa utawala wa Saddam Hussein lakini hilo lilimazika baada ya vyama vya washia na wakurdi kushiriki katika uchaguzi wa januari 30.