BAGHDAD:Watu watatu wanyongwa Iraq
1 Septemba 2005Leo Iraq imewanyonga watu wa watatu wa waliokuwa wameshtakiwa kwa mauaji hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa serikali hiyo kutekeleza hukumu ya kifo tangu kuanguka kwa utawala war ais Saddam Hussein wa nchi hiyo.
Bayan Ahmed Said,Ouday Dawood Salman na Dhahar Jasim Hassan wamenyongwa baada ya hukumu yao kutiwa saini na rais wa Iraq.
Watatu hao walipatikana na hatia ya mauaji,utekaji nyara na ubakaji na mahaka ya mkoa wa Wasit kusini ya Iraq.
Imeripotiwa kwamba kutekelezwa kwa hukumu hiyo huenda ikafungua njia ya hukumu sawa na hiyo kutekelezwa dhidi ya Saddam Hussein na wasaidizi wake wanaosubiri kushtkiwa.
Rais Gorge Bush anaunga mkono hukumu ya kifo na amesema angependelea hukumu hiyo ichukuliwe dhidi ya Saadam iwapo atakutikana na hatia katika kesi inayotarajiwa kuanza baadae mwaka huu.