BAGHDAD:Watu wameendelea kuuawa nchini Iraq kutokana na mashambulio ya mabomu.
15 Septemba 2005Mfululizo wa mashambulio ya mabomu umeendelea kuutikisa mji mkuu wa Iraq Baghdad na kusababisha watu 25 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa leo hii.
Katika shambulio la karibuni kabisa,waripuaji wawili wa kujitoa muhanga,walifanikiwa kushambulia msafara wa doria wa polisi katika wilaya ya Dura kusini mwa Baghdad na kuwauwa askari polisi tisa.
Watu 16 wengine waliuawa saa chache baada ya kutokea shambulio hilo la awali,ambalo nalo lilielekezwa katika msafara wa doria wa polisi wilani Dura.
Mashambulio haya ya leo yanafuatia yaliyofanyika jana ambayo yalihusisha miripuko ya mabomu na ufyatuaji wa risasi,ambapo watu zaidi ya 150 waliuawa na wengine kwa mamia walijeruhiwa.
Katika ujumbe wake uliotumwa kwa njia ya tuvoti,kiongozi wa kikundi cha Al-Qaeda nchini Iraq,Abu Musab al-Zarqawi,alisikika akisema kuwa ameanzisha vita na Washia walio wengi nchini humo.