BAGHDAD:Watu takriban 30 wauwawa Iraq
18 Septemba 2005Matangazo
Watu takriban 30 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mripuko wa bomu uliotokea katika soko moja karibu na mji mkuu wa Iraq Baghad hapo jana jioni.
Maafisa wa wizara ya mambo ya ndani nchini humo wamearifu kuwa mashambulio hayo yamefanyika kwenye wilaya inayokaliwa na washia wengi.
Zaidi ya watu 200 wameuwawa kwenye mashambulio ya mabomu na ufyatuliaji risasi ndani na nje ya mji wa Baghdad wiki hii.