BAGHDAD:Wanamgambo washambuliwa vikali Iraq
5 Oktoba 2005Matangazo
Vikosi vya Marekani vikisaidiwa na majeshi ya Kiiraqi,vimefanya mashambulio makubwa kabisa ya mwaka huu dhidi ya vituo vinavyoshukiwa kuwa ni vya wanamgambo,magharibi mwa Iraq.Inasemekana kuwa kiasi ya wanajeshi 2,500 wa vikosi maalum vya Kimarekani wanashiriki katika operesheni hii,wakisaidiwa na helikopta na ndege za kivita.Kwa wakati huo huo mashambulio ya wanamgambo waliojitolea muhanga yanaendelea katika mji mkuu Baghdad.Katika shambulio la hivi karibuni,Wairaqi 3 waliuawa na wengine 6 walijeruhiwa baada ya gari iliyopakiwa bomu kuripuliwa katika uwanja wa majengo ya serikali na mwanamgambo aliejitiolea kufa.