BAGHDAD:Wanajeshi saba wa Majini wa Marekani wauwawa Iraq
3 Agosti 2005Matangazo
Taarifa kutoka nchini Iraq zimerifu wanajeshi saba wa majini wa Marekani wameuwawa katika mashambulio mawili ya mabomu huko magharibi mwa mji wa Baghdad.
Wanajeshi wa Marekani wapo kwenye eneo hilo ili kujaribu kuzifunga njia za mpaka mkubwa zinazotumiwa na wapiganaji wakigeni kuingia nchini Iraq.
Mauaji hayo yamefikisha idadi ya wanajeshi waliokufa nchini humo kuzidi 1800.