BAGHDAD:Wafungwa 500 kuachiliwa Iraq
7 Januari 2004Matangazo
Utawala unaoongozwa na Marekani nchini Iraq unapanga kuwaachilia huru wafungwa 500 kutoka katika makambi inakowashikilia katika kile kinachoonekana kuwa ni kuonyesha nia njema.
Wakati huo huo itatowa bakshishi kwa Wairaq 30 wanaotafutwa katika uasi dhidi ya Marekani.Kwa mujibu wa maafisa wa jeshi la muungano kuachiliwa kwa wafungwa huo pia kunakusudia kukuza taarifa za kijasusi ambazo zimezidi kuongezeka katika kipindi cha wiki tatu tokea kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein.Wengi wa wafungwa wanaotarajiwa kuachiliwa ni watuhumiwa wa ngazi ya chini washirika wa uasi ambao hawahusiki moja kwa moja katika mashambulizi dhidi ya vikosi vya muungano.
Kuachiliwa huru kwa Wairaq wanaoshikiliwa kwa muda usiokuwa na kikomo na bila ya kufunguliwa mashtaka limekuwa dai kuu la wananchi wa nchi hiyo na viongozi wa makabila pamoja na watetezi wa haki za binaadamu.