BAGHDAD:Vita dhidi ya magaidi vyaimarishwa Iraq
5 Novemba 2005Matangazo
Vikosi vya Kimarekani nchini Iraq katika vita vyake dhidi ya mtandao wa kigaidi wa al Qaeda,vimeanzisha mashambulio makubwa karibu na eneo linalopakana na Syria.Mashambulio hayo hasa yanaelekezwa mji wa Husaiba katika wilaya ya Anbar magharibi mwa Iraq.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya Marekani,hadi wanajeshi 2,500 wa Kimarekani wanashiriki katika operesheni hiyo yenye azma ya kuwangóa wanamgambo wanaojificha katika eneo hilo la mpakani na pia kuboresha usalama katika sehemu hizo kabla ya kufanywa uchaguzi wa bunge mwezi ujao.Vikosi vya Marekani vinasaidiwa na hadi wanajeshi 1,000 wa Kiiraqi.Ripoti zingine zinaarifu kuwa katika mashambulio yaliyofanywa na waasi kusini na magharibi ya mji mkuu Baghdad,wanajeshi 2 wa Kimarekani wameuawa.