Baghdad:Umwagikaji damu waendelea nchini Iraq
16 Mei 2005Matangazo
Nchini Iraq maafisa wanne wa polisi na raia wawili wameuwawa mapema hapo jana katika mashambulio mawili ya mabomu dhidi ya msafara wa maafisa wa serikali katika mji wa Baquba.
Wakati huo huo wafanyikazi wa Manispaa wameipata miili 30 ya watu waliouwawa,katika mji uliopo nje ya Bghadad
Kwengineko wanajeshi wa Marekani wamesema oparesheni kali dhidi ya waasi iliyoanza wiki iliyopita imemalizika salama wa salmini.
Katika Oparesheni hiyo wanejeshi wa Marekani wamesema wamewauwa zaidi ya waasi 125 huku wanajeshi wao 9 wakipoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa
Oparesheni hiyo ndio kali zaidi kuwahi kufanywa na Marekani dhidi ya waasi tangu uvamizi wa majeshi ya marekani huko Falluja.