BAGHDAD:Shambulio la bomu lauwa watu 16 mjini Basra,Iraq.
8 Septemba 2005Shambulio la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari kusini mwa Iraq katika mji wa Basra,limesababisha watu 16 kuuawa na mwengine 20 kujeruhiwa.Shambulio hilo limetokea nje ya mkahawa mmoja katika mji huo ambao ni ngome ya Washia,ambao kwa muda sasa umekuwa kimya kulinganisha na mikoa mingine ya kaskazini mwa Iraq.
Wakati huo huo wanajeshi wa Marekani,wamemuokoa mkandarasi mmoja wa Kimarekani,aliyekuwa anashikiliwa mateka kwa kipindi cha miezi kumi sasa.Taarifa iliyotolewa na maofisa wa jeshi la Marekani,imemtaja mkandarasi huyo kuwa ni Roy Hallum na alikuwa na afya njema.
Alikutwa katika sehemu moja ya mashambani isiyokaliwa na watu,kiasi cha maili 15 kusini mwa Baghdad pamoja na mateka wengine raia wa Iraq.
Hallum alitekwa nyara na watu waliokuwa na silaha wakati akiwa ofisini kwake mjini Baghdad mwezi wa Novemba mwaka jana.