BAGHDAD:Saddam Hussein ahojiwa na mahakama maalum ya Iraq
13 Juni 2005Matangazo
Mahakama maalum nchini Iraq inayochunguza kesi dhidi ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein, imesema Jaji wa Iraq amemhoji kiongozi huyo juu ya mauaji ya wanaume wengi katika kijiji cha washia ambako aliponea chupu chupu jaribio la kumuua mwaka 1982.
Mahakama hiyo pia imetoa kanda ya video ikimuonyesha Saddam na washirika wake katika utawala wake wakihojiwa.
Mauaji yaliyofanywa mjini Dujail ni mojawapo ya uhalifu anaotuhumiwa kuufanya kiongozi huyo lakini kumekuwepo na madai kwamba huenda baadhi yayo yakatumika katika kesi dhidi yake.
Serikali ya Iraq imesema ingependa kumfikisha mahakamani katika muda wa miezi michache kabla ya uchaguzi lakini maafisa wa mahakama wamesema hakuna ratiba iliyotolewa.