BAGHDAD:Rumsfeld afanya ziara ya ghafla Iraq
12 Julai 2006Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld amefanya ziara ya ghafla nchini Iraq. Ziara hii inafanyika huku kukizuka maswali mengi nchini Marekani juu ya vita vya Iraq na lini wanajeshi wake wataanza kurudi nyumbani.
Hata hivyo bwana Rumsfeld ambaye alizuru pia Afghanstan na Tajikistan amekataa kuzungumzia juu ya masuala ya kijeshi.
Bwana Rumsfeld atajadiliana na waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki juu ya masuala ya usalama pamoja na suala la kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Iraq.
Wakati huo huo shmbulio la bomu limefanyika katika soko moja huko mashariki mwa mji wa Baghdad na kuwauwa watu watano na wengine 15 wakajeruhiwa.