Baghdad.Rais wa Iraq azionya nchi za nje kuacha kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.
26 Septemba 2006Matangazo
Rais wa Iraq Jalal Talabani ameyaonya mataifa ya kigeni kuacha kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.
Katika mahojiano na radio ya taifa ya Marekani, rais Talabani amezitaja Syria, Uturuki na Iran akisema zinabidi ziheshimu mamlaka na uhuru wa Iraq.
Rais wa Iraq amesema la sivyo Baghdad itajibu kwa namna hiyo hiyo kwa kuunga mkono upinzani wa nchi hizo.
Rais wa Marekani Goerge W. Bush amezitolea mwito Syria na Iran zizuie mikururo ya wanamgambo wanaopitia katika mipaka yao.