BAGHDAD:Operesheni kali ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya waasi mjini Qaim Iraq
17 Juni 2005Matangazo
Katika mzozo wa Iraq watu kadhaa wameuwawa kwenye mlipuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari lililofanywa nje ya msikiti mmoja mjini Baghdad.
Kwengineko nchini humo wanajeshi wa Marekani wameanzisha kali dhidi ya ya waasi katika mji wa Qaim karibu na mpaka wa Syria.
Wanajeshi kiasi cha elfu moja wanahusika katika operesheni hiyo ambayo Marekani inasema inalenga kuwamaliza wapiganaji wakigeni waliomo nchini Iraq.
Wakazi wa eneo hilo wamesema mashambuliano ya risasi yaliyoendelea usiku kucha bado yanaendelea.Waasi 40 wameuwawa na mashambulio ya anagani yanayofanywa na wanajeshi hao wa Marekani.