BAGHDAD:Nakala za katiba mpya zimeanza kusambazwa Iraq
7 Oktoba 2005Zikiwa zimesalia siku kumi kufikia kura ya maoni juu ya katiba wairaq leo wameanza kupewa nakala ya katiba hiyo.
Wakaazi wa mjini Baghdad na miji mengine wamepokea nakala hizo ijapokuwa baadhi ya watu walikataa kuzichukua nakala hizo wakihofia mashambulio ya waasi waliopania kuvuruga kura hiyo ya maoni Oktoba 15.
Takriban nakala milioni 5 za katiba hiyo zilipelekwa Iraq mnamo jumatatu lakini usambazaji wa nakala hizo unaelekea haujaanza katika maeneo ya Kaskazini na kusini ambako katiba hiyo inatarajiwa kukubaliwa kwa urahisi kwenye kura ya maoni.
Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Bulgaria ametangaza kwamba wanajeshi wa nchi hiyo wataendelea kubakia Iraq hadi uchaguzi wa Desemba ufanyike lakini wataanza kuondoka nchini humo kufikia mwishoni mwa mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa.