BAGHDAD:Mzozo wa Iraq waasi 10 wauwawa
26 Mei 2005Matangazo
Watu wasiopungua kumi wanaoushukiwa kuwa waasi nchini Iraq akiwemo kiongozi mmoja wa kundi la kidini wameuwawa katika mji wa Hadhitha katika operesheni dhidi ya waasi iliyoanzishwa kwa pamoja na wanajeshi wa Marekani na Iraq.
Mapambano makali yalizuka hapo jana baada ya wanajeshi hao kuingia katika mji huo kuwasaka waasi.
Wakati huo huo wapiganaji wametoa taarifa kupitia mtandao wa Internet kwamba kiongozi wa kundi la Alqaeda nchini Iraq Abu Musab AL Zarqawi amejeruhiwa mbavuni kwa risasi.
Zaqawi inasemekana alipigwa risasi wekendi iliyopita katika mji wa Ramadi katika operesheni ya wanamaji wa Marekani na vikosi vya usalama vya Iraq.