BAGHDAD:Mshauri wa waziri mkuu wa Iraq Auwawa Baghdad
23 Mei 2005Matangazo
Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wamemuua mshauri wa waziri mkuu Ibrahim Al Jafaari.
Polisi wanasema Wael Rubaie pamoja na dereva wake waliuwawa mjini Baghdad.
Wakati huo huo bomu lilolokuwa limetegwa ndani ya gari limeripuliwa karibu na msafara wa afisa wa kikurdi katika mji wa Tuz Khurmatu kusini mwa Kirkuk.
Takriban watu wanne wameuwawa katika shambulio hilo na wengine 16 wamejeruhiwa.
Jeshi la Marekani pia limethibitisha kwamba wanajeshi wake wanne wameuwawa katika mashambulio yaliyofanywa kwenye miji ya Mosul na Tikrit.