BAGHDAD:Mjumbe wa Misri aliyetekwa nyara nchini Iraq auwawa
8 Julai 2005Mjumbe wa Misri nchini Iraq aliyekuwa ametekwa nyara jumamosi iliyopita nchini humo ameuwawa.
Serikali ya Misri imethibitisha taarifa za kuwawa kwa Ihab El Sharif na kundi lilokuwa limemteka nyara la wapiganaji linalodai kuhusiana na mtandao wa kigaidi wa Alqaeda nchini Iraq.
Sharif alitekwa nyara katika barabara mjini Baghdad siku kadha baada ya serikali ya Iraq kutangaza kwamba Misri ina mipango ya kumfanya Sharif balozi kamili wa Misri nchini Iraq.
Kwengineko nchini Iraq watu watatu wameuwawa na zaidi ya wengine 50 wamejeruhiwa katika mashambulio ya makombora dhidi ya nyumba na maduka mjini Mosul.
Watu wengine 13 wameuwawa na 13 kujeruhiwa kwenye mashambulio mengine mawili ya mabomu ya kutegwa ndani ya gari katika mji wa Jabala kusini mwa Baghdad.