BAGHDAD:Mashambulio yanaendelea nchini Iraq
20 Juni 2005Matangazo
Mashambulio ya waasi nchini Iraq yanaonekana kupamba moto licha ya kuanzishwa kwa operesheni kali dhidi yao na wanajeshi wa Marekani pamoja na vikosi vya uslama vya Iraq.
Takriban watu 11 wameuwawa na zaidi ya 50 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari katika mji wa kikurdi wa Arbil kaskazini mwa Iraq mapema leo asubuhi.
Hapo jana takriban watu 26 waliuwawa na wengine kiasi cha 30 kujeruhiwa katika mripuko wa bomu la kujitoa muhanga mjini Baghdad.
Operesheni ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya waasi kwenye mpaka wa Syria na Iraq imepelekea kuwawa kwa zaidi ya waasi 50.