BAGHDAD:Mashambulio ya wanajeshi wa Marekani yawauwa watu 45 Iraq
31 Agosti 2005Matangazo
Watu wasiopungua 45 wameuwawa nchini Iraq kufuatia mashambulio ya angani yaliyofanywa na wanajeshi wa Marekani katika mji wa Karbila karibu na mji wa Qaim mpakani mwa Syria.
Msemaji wa jeshi la Marekani amearifu kamanda mmoja wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda Abu Islam pamoja na washukiwa kadhaa wa ugaidi wameuwawa katika mashambulio hayo.
Akidhibitisha juu mashambulio hayo msemaji wa jeshi la Marekani amesema ndege hizo za Marekani zilifanya mashambulio matatu na zililenga majengo yanayodhaniwa kuwa maficho ya wapiganaji wa kundi la mtandao wa kigaidi wa Alqaeda ama vikundi vingine vya magaidi nchini Iraq.