BAGHDAD:Katiba mpya ya Iraq yapigiwa kura
15 Oktoba 2005Matangazo
Wairaqi hii leo wanapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya nchi yao.Ulinzi umeimarishwa kote Iraq na mipaka imefungwa isipokuwa kwa misafara iliyo ya lazima.Hatua hiyo imechukuliwa katika juhudi ya kuzuia mashambulizi ya wanamgambo dhidi ya wapiga kura.Kundi la Al Qaeda nchini Iraq limelaani kura hiyo ya kihistoria na limetoa wito kwa Waarabu wa madhehebu ya Kisunni walio wachache,wasuse kupiga kura.