BAGHDAD:Katiba mpya ya Iraq bado ni kitendawili tega
25 Agosti 2005Matangazo
Hatua ya mwisho ya kuandika katiba mpya ya Iraq imefikiwa.
Katiba hiyo inatarajiwa kupitishwa na bunge jioni hii hata hivyo lakini mazungumzo yanaendelea.
Msemaji wa serikali Laith Kubba amewaambia waandishi habari kwamba bunge halihitaji kukutana rasmi ili kuipitisha katiba hiyo kwasababu tayari liliiipasisha katiba hiyo jumatatu iliyopita.
Wasunni ambao wanaendelea kushikilia msimamo wao wa kuikataa katiba hiyo wamesema huenda ikazusha vita vya wenya kwa wenyewe.
Kwa mujibu wa mwanachama wa sunni kwenye jopo hilo la katiba amesema iwapo kipengele cha kuwepo serikali ya shirikisho hakitaondolewa basi hakuna haja ya kuwepo katiba hiyo.