Baghdad.Bomu la kujitolea muhanga lauwa 18 nchini Iraq.
8 Septemba 2006Matangazo
Waasi nchini Iraq wamewauwa kiasi cha watu kumi na nane na kuwajeruhi kiasi cha sitini, kufuatia bomu la kujitolea muhanga katika mji mkuu Baghdad.
Bomu hilo limetokea wakati waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki kusaini makubaliano na kamanda wa kijeshi wa Marekani Generali George Casey juu ya jeshi la Iraq kuanza kuchukua nafasi ya ulinzi uliokuwa chini ya amri ya Marekani.
Makubaliano hayo yanampa Maliki fursa ya kuendesha operesheni za kijeshi za anga na majini.