BAGHDAD:Bomu la gari limeua watu 25 nchini Iraq
30 Oktoba 2005Matangazo
Si chini ya watu 25 wameuawa na wengine 40 wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea nchini Iraq.Mripuko huo ulitokea jioni katika mji wa Howaider ulio na wakazi wengi wa madhehebu ya Kishia,wakati ambapo watu walikuwa wakifuturu. Serikali ya Iraq ikisaidiwa na majeshi ya Kimarekani,inapambana na mashambulio ya waasi nchini humo na hulaumu makundi mbali mbali likiwemo pia kundi la Al Qaeda kuwa ndio yanayohusika na mashambulio nchini Iraq.