Baghdad.Abu Rana kiongozi wa al-Qaida akamatwa nchini Iraq.
4 Septemba 2006Matangazo
Maafisa nchini Iraq wamemkamata wamemkamata kiongozi wa kundi la al-Qaida nchini humo.
Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama kwamba, Hamed Jumaa al-Saed, anaetambulika pia kama Abu Human ama Abu Rana alikamatwa siku chache zilizopita akiwa amejificha katika nyumba ya wananchi kusini magharibi mwa Baquba.
Al-Saed anashtumiwa kwa kupanga shambulio la mabomu mwezi February katika maeneo ya washia huko Samarra.
Akizungumzia furaha yake kutokana na kukamatwa kwa kiongozi huyo, naibu Waziri Mkuu wa Iraq Barhim Salih amesema.
“ Natumai kwamba hii itakuwa ni dalili ya kutosha kwa watu kwamba serikali ya Iraq kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa na jeshi mchanganyiko wa mataifa, hatutaacha kupambana na magaidi”.