BAGHDAD: Zaidi ya watu 45 wauwawa Arbil nchini Iraq
4 Mei 2005Watu 45 wameuwawa na wengine 90 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga lililofanywa mjini Arbil Kaskazini mwa Iraq. Arbil ni mji uliopo chini ya Masoud Barzani kiongozi wa chama cha wakurdi ambacho ni kimojawapo katika makundi mawili makubwa ya wakurdi nchini Iraq. Tukio hilo limekuja siku moja baada ya .Serikali mpya ya Iraq kuapishwa hapo jana huku nyadhifa tano muhimu za mawaziri na nyadhifa mbili za manaibu zikisalia wazi na hivyo kuonyesha ugumu uliopo wa kuunda uongozi unaounganisha washia,wasunni na wakurdi.
Hadi kufikia sasa waziri mkuu Ibrahim Al Jafaari ameshindwa kuwachagua mawaziri wa mafuta,Ulinzi,viwanda,umeme,na haki za binadamu.
Kwengineko mjini Baghdad waasi wamemuua kwa kumpiga risasi afisa mwandamizi katika idara ya maji. Wanajeshi wa Marekani wamesema wakishirikiana na vikosi vya Iraq wamewaua waasi 12 katika kituo cha kukagua magari cha ramadi magharibi mwa mji wa Baghdad.
Wakati huo huo wanajeshi wa Marekani wamesema wameipata maiti ya rubani wa ndege yao ya k