BAGHDAD-Wimbi la mashambuli ya kujitoa muhanga yanazidi kuteketeza maisha ya watu nchini Iraq.
11 Mei 2005Wimbi la mauaji yanayoendeshwa na waasi nchini Iraq kwa kutumia mabomu ya kujitoa muhanga leo hii limesababisha kuuliwa kwa watu 56.Shambulio kubwa limetokea katika mji wa Tikrit,ambapo mtu aliyekuwa ndani ya gari alijiripua akiwa katikati ya kundi la watu,wengi wakiwa wafanyakazi wahamiaji wa madhehebu ya Shia.
Polisi wa Iraq wameeleza kuwa watu 27 wameuawa katika shambulio hilo.
Katika mji wa Hawija kusini-magharibi mwa Kirkuk,mtu mmoja aliyekuwa amejisheni mabomu mwili mwake,aliingia katika kituo cha kupokelea wanajeshi wapya na kujiripua,akicha watu 19 wamekufa na wengine 25 wamejeruhiwa.
Bomu jingine la kujitoa muhanga limeripuka nje ya kituo cha polisi kusini mwa Baghdad katika kitongoji cha Dora na kuuwa watu wanne na kujeruhi wengine kadhaa.